WARSAW, Poland
SAFARI za ndege takribani 10 zimehairishwa kutokana na taarifa za kuwapo kwa uwezekano wa mlipuko wa bomu katika Uwanja wa Ndege wa Warsawa nchini Poland.
Baada ya taarifa za tishio, mamlaka za usalama zilianza upekuzi wa kina kwenye Uwanja wa Ngege huo lakini hazikubaini uwepo wa bomu lililotegwa.
Shirika la Ndege la Jamhuri ya Ireland limetajwa kuathirika Zaidi baada ya kuhairisha safari zake nne kwenda maeneo mbalimbali duniani.
Kabla ya hiki kilichotokea Poland, taarifa za viwanja vya ndege vya Ulaya kuwekewa mikakati ya kulipuliwa kwa mabomu zilisika pia nchini Uingereza.
Mapema wiki hii, polisi wa kimataifa wa jijini London walithibitisha kupokea taarifa za tishio la bomu katika Uwanja wa Ndege wa Heathrow.
Sambamba na hilo, pia taarifa ya polisi ilieleza kuwa kulikuwapo na tishio la bomu katika Uwanja mwingine wa Ndege wa Manchester.
Hata hivyo, baada ya ukaguzi, polisi walijiridhisha kuwa hakukuwa na hatari yoyote katika viwanja vyote viwili, bali ulikuwa ni ujumbe wa tishio tu.


