10.5 C
New York

Messi hakabiki, aandika historia mpya MLS

Published:

MIAMI, Marekani

MSHAMBULIAJI wa Inter Miami, Lionel Messi, amekuwa mchezaji wa kwanza wa Ligi Kuu ya Marekani [MLS] kutwaa misimu miwili mfululizo tuzo ya Mfungaji Bora.

Mshindi huyo mara nane wa tuzo ya Ballon d’Or ameibeba tena msimu huu baada ya kufunga mabao 26 katika mechi 31.

Kwa idadi hiyo, anamzidi mabao manne straika wa FC Dallas, Peter Musa, pia akimwacha matano Sam Surridge wa Nashville.

Messi anakuwa mchezaji wa sita katika historia ya MLS kuinyakua mara mbili tuzo hiyo. Miongoni mwa waliowahi kufanya hivyo ni nyota wa zamani wa Southampton, Bradley Wright-Phillips.

Mbali na kufunga mabao 26, pia Muargentina huyo mwenye umri wa miaka 39 ametoa ‘asisti’ 17 msimu huu wa MLS.

Related articles

Recent articles