14.2 C
New York

Havertz avunja rekodi ya kuotea Arsenal

Published:

LONDON, Uingereza

KUFIKIA hatua hii ya msimu, straika wa Arsenal, Kai Havertz, ndiye mchezaji wa timu hiyo aliyenaswa mara nyingi kwenye eneo la kuotea [offside].

Mjerumani huyo amekutwa ‘offside’ mara 15, idadi kubwa zaidi, ikilinganishwa na Bukayo Saka aliyenasa mara 14 kwa kipindi chote cha msimu uliopita.

Havertz amekuwa akikosolewa kwa kukosa mwendelezo wa kiwango kizuri, lawama ambazo pia amekuwa akitupiwa straika mwingine wa timu hiyo, Viktor Gyokeres.

Kwa pamoja, wawili hao wamefunga mabao matatu na kutoa ‘asisti’ moja pekee msimu huu wa Ligi Kuu ya England [EPL].

Hata hivyo, licha ya ubutu wao kwenye eneo la ushambuliaji, Arsenal imeshinda mechi tisa kati ya 10 ilizocheza hadi sasa.

Related articles

Recent articles