19.1 C
New York

Wafungwa 548 wanusurika kunyongwa

Published:

CALIFORNIA, Marekani

WAFUNGWA 548 waliokuwa wakisubiri kunyongwa wamebadilishiwa hukumu na sasa watasota gerezani kwa kipindi chote cha maisha yao.

Msamaha huo wa Gavana wa Jimbo la California, Gavin Newsom, unakuja siku chache tu baada ya kumalizika kwa Uchaguzi mdogo nchini Marekani.

Hata hivyo, hii si mara ya kwanza kwa California kutengua adhabu ya kifo kwani hakuna mfungwa aliyenyongwa katika Jimbo hilo tangu mwaka 2006.

Kwa mujibu wa takwimu, ni wafungwa 13 pekee waliowahi kunyongwa tangu zilipopigwa kura za kupinga hukumu ya kifo mwaka 1978.

Wakati huo huo, hatua ya sasa ya kiongozi huyo wa Democrat, Newsom, imetafsiriwa kuwa ni mkakati wake wa kugombea kiti cha urais katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2028.

Related articles

Recent articles