20.3 C
New York

Mtoto wa Zidane apigwa ‘panga’ Algeria

Published:

ALGIERS, Algeria

MLINDA mlango wa timu ya soka ya Taifa ya Algeria, Luca Zidane, hajaitwa kwenye kikosi kinachojiandaa kuivaa Togo kwenye mechi za kufuzu fainali za AFCON za mwaka 2027.

Luca, ambaye ni mtoto wa staa Zinedine Zidane, amekosekana kwenye mechi za hivi karibuni kutokana na majeruhi na adhabu ya kufungiwa michezo miwili.

Kwa mujibu wa kocha wa Algeria, Brahim Hemdani, uamuzi wa kumwacha safari hii umetokana na sababu za kiufundi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Hemdani amesema: “Nahitaji makipa watatu wanaopata nafasi ya kucheza mara kwa mara.”

Katika chaguo lake kwa makipa, kocha huyo amewaita Oussama Benbot wa USM Alger, Melvin Mastil wa Lausanne-Sport ya Uswis na Abdelatif Ramdane anayekipiga MC Alger.

Related articles

Recent articles