LAGOS, Nigeria
BAADHI ya wasanii wa muziki nchini Nigeria hutumia ushirikina kupata ngoma kali zinazofanya vizuri ndani na nje ya Afrika.
Aliyesema hayo ni rapa maarufu wa Nigeria, Tochukwu Ojogwu, wengi wakimfahamu kwa jina la Odumodublvck.
Odumodublvck amesema ni ngumu kupata wimbo unaofanya vizuri na baadhi ya wanamuziki hawajahi kufanikiwa katika hilo kwa miaka yao yote kwenye kiwanda.
Aidha, mshikaji huyo aliwapongeza Burna Boy, Wizkid na Davido kwa kuwa na mwendelezo mzuri wa kuachia ngoma zinazotamba.
“KUpata wimbo mkubwa si kazi rahisi. Wakati mwingine watu wanakwenda kwa waganga ili kupata wimbo mkubwa,” amesema Odumodublvck.


