MILAN, Italia
STRAIKA wa AC Milan, Goncalo Ramos, amedai kuwa yeye ndiye anayestahili kuanza kwenye kikosi cha timu ya soka ya Taifa ya Ureno.
Ramos ameyasema hayo licha ya nahodha wa kikosi, Cristiano Ronaldo, kurejea kikosini kwa ajili ya mechi za Ligi ya Mataifa ya Ulaya [Nations League] zitakazochezwa Novemba, 2026.
Ikumbukwe, Ramos [25] amekuwa akitumika Zaidi kikosini wakati Ronaldo akiwa hayupo, akianza katika mechi zote tatu zilizopita.
“Nataka kuwa mchezaji wa kikosi cha kwanza wa timu ya taifa. Nimeshasema wazi, kwamba kama kuna mtu anayestahili kuanza, basi ni mimi. Kocha na nchi nzima wanaweza kuliona hilo,” amesema.
Hata hivyo, mshambuliaji huyo ameweka wazi kuwa kauli yake hiyo hailengi kumdharau Ronaldo au kutaka aachwe benchi.


