18.3 C
New York

Kipa aliyemuua mshambuliaji akiona cha moto

Published:

MADRID, Hispania

BAADA ya kugongana na Jesus de Miguel na kusababisha kifo cha mshambuliaji huyo wa Tenerife, kipa wa FC Andorra, Jesús Owono, amekumbana na wakati mgumu huko mitandaoni.

Owono raia wa Guinea ya Ikweta, aligongana na straika huyo mwenye umri wa miaka 30 wakati timu zao zilipovaana katika mchezo wa Ligi Daraja la Pili nchini Hispania uliochezwa Jumatano ya wiki hii.

Wakati timu hizo zikiwa sare ya mabao 2-2, De Miguel alifukuzia mpira mrefu ulioingia kwenye boksi la FC Andorra na ndipo Owono alipomvaa na kumngonga kifuani kwa goti lake.

Kwa tukio hilo, Owono alilimwa kadi nyekundu, wakati De Miguel akipata matibabu, kabla ya kukimbizwa hospitali na kisha kufariki jana [Novemba 30, 2026].

Katika mitandao, mlinda mlango huyo amekumbana na maneno ya kashfa, matusi na wengi wakienda mbali zaidi kwa kumwita muuaji.

Kwa rafu yake dhidi ya De Miguel, Owono anatarajiwa kufungiwa mechi kati ya nne hadi 12.

Related articles

Recent articles