Na Hassan Mwasha, Gazetini
UKIACHA Yanga yenye watano, Azam FC ndiyo timu nyingne yenye idadi hiyo ya wachezaji walioitwa kwenye kikosi cha Taifa Stars kinachojiandaa kuivaa Nigeria ‘Super Eagles’.
Stars itaifuata Super Eagles katika Uwanja wa Kimataifa wa Godswill Akpabio mjini Uyo, Nigeria, mchezo wa kufuzu AFCON 2027 utakaochezwa Novemba 17, 2026.
Kocha wa Stars, Miguel Gamondi, ameita ‘jeshi’ lake kuelekea mchezo huo wa kuwania tiketi ya kushiriki fainali zijazo za AFCON za mwaka 2027.
Katika kikosi hicho, Yanga ina wachezaji watano, ambao ni Ibrahim Bacca, Dickson Job, Bakari Nondo, Suleiman Mwalim na Clement Mzize.
Kwa upande wao, Azam ina uwakilishi wa Aishi Manula, Zuber Foba, Abdul Hamis, Himid Mao na Feisal Salum ‘Fei Toto’.
Wachezaj pekee wawili wa Wekundu wa Msimbazi walioingia kwenye kikosi cha Gamondi safari hii ni Anthony Mligo na Nathaniel Chilambo.
Baadhi ya nyota wa kigeni waliojumuhishwa kikosini ni Novatus Miroshi [Goztepe, Uturuki], Cyprian Kachewele [Kryvbas, Ukraine] na Bernard Kamongo [FC Dallas, Marekani].
Stars watashuka dimbani kwa mechi yao ya tatu ya kufuzu AFCON 2027 baada ya kufungwa mabao 2-0 na Guinea-Bissau na sare ya bao 1-1 dhidi ya Madagascar.


