8.5 C
New York

Maduka yavunjwa vurugu Ujerumani

Published:

MUNICH, Ujerumani

RAIA wa Ujerumani walioingia mitaani kwa maandamano wamesababisha uharibifu mkubwa wa mali, ikiwamo kuvunja maduka mjini Frankfurt jana Oktoba 31, 2026.

Maandamano hayo ya kupinga kupanda kwa gharama za maisha yameshuhudiwa pia katika miji mingine, huku polisi wakilazimika kuingilia kati kwa mabomu ya machozi na maji ya kuwasha.

Mbali na Frankfurt, miji mingine mikubwa ya kibiashara iliyoshuhudia maandamano hayo ni Berlin, Cologne na Hamburg.

Aidha, polisi wameeleza kuwa wamelazimika kutumia nguvu ya wastani kukabiliana na waandamanaji waliorusha mawe na chupa.

Mbali na ugumu wa maisha, maandamano hayo yanaongozwa na kaulimbiu ya ‘Gen Z regelt’ [Gen Z takes charge] yanalalamikia bajeti ndogo kwenye huduma za kijamii, hasa elimu.

Ujerumani inaungana na mataifa mengine ya Ulaya, ikiwamo Ufaransa, ambako wananchi wanalalamikia kupanda kwa gharama za maisha.

Kwa upande wa Ufaransa, kampeni iliyoongozwa na vijana ilisababisha watu zaidi ya 320,000 kuingia baraarani jana.

Related articles

Recent articles