11.7 C
New York

Polisi aliyerushiwa bomu apata utetezi

Published:

PARIS, Ufaransa

WAENDESHA mashitaka nchini Ufaransa wanachunguza tukio la polisi mmoja kurushiwa bomu la petroli wakati wa maandamano.

Maandamano hayo ya wiki kadhaa sasa yametokana na kile wananchi walichodai kuwa wamechoshwa na kupanda kwa gharama za maisha.

Aidha, uchunguzi huo unatokana na video inayomuonesha ofisa wa polisi akiugulia maumivu huku mguu wake ukiwa unaungua moto wakati maandamano yakiendelea juzi jijini Paris.

Wakati huo huo, polisi huyo aliyepata majeraha makubwa kwenye kifundo cha mguu na mkononi, ameliambia Gazeti la Le Figaro la Ufaransa kwamba alirushiwa bomu.

Kwa upande wake, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Laurent Nunez, amekiita kitendo hicho kuwa ni jaribio la kuua dhidi ya polisi aliyekuwa akitekeleza majukumu yake.

Related articles

Recent articles