11.7 C
New York

Bellingham afikisha mabao 50 Madrid

Published:

MADRID, Hispania

KIUNGO wa Real Madrid, Jude Bellingham, amefikisha mabao 50 tangu alipojiunga na timu hiyo akiwa na umri wa miaka 19.

Bellingham alitua Madrid mwaka 2023 akitokea Borussia Dortmund, ambapo usajili wake uligharimu kitita cha Pauni milioni 88.5.

Katika mechi ya jana Novemba Mosi, 2026, Muingereza huyo alifunga bao lake la 50 na kuiwezesha Madrid kushinda mabao 3-0 dhidi ya Racing Santander.

Madrid wakiwa ugenini walipata bao lao la kwanza katika dakika ya 11, mfungaji akiwa ni Kylian Mbappe aliyepiga penalti baada ya Matteo Prati kumuangusha kwenye boksi.

Bellingham alifunga bao la pili kwa Madrid katika dakika ya 21, kabla ya mchezaji ghali, Yan Diomande, kuongeza jingine na kuipa Madrid uhakika wa kuondoka na pointi tatu.

Related articles

Recent articles