15 C
New York

Waliofariki kwa Ebola wafikia 5,000

Published:

KINSHASA, DRC

TAKWIMU za Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo [DRC] zimeeleza kuwa watu zaidi ya 5,000 wamepoteza maisha kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola.

Ripoti hiyo inaeleza pia, majimbo nane kati ya 26 yameathiriwa na ugonjwa huo, huku maambukizi yakiwa ni zaidi ya 10,300.

Mlipuko wa Ebola nchini DRC ulianza Mei, 2026, lakini hali ilikuwa mbaya kuwahi kutokea ilipofika Agosti, kwa mujibu wa Wizara ya Afya.

Kwa mujibu wa takwimu, uwezekano wa kifo kutokana na Ebola ni mkubwa kwa sasa, sawa na wastani wa asilimia 48.6.

Hivi karibuni, Wizara ya Afya ilieleza kuwa bado Jimbo la Ituri ndiyo kitovu cha maambukizi. Eneo hilo liko Kaskazini-Mashariki mwa DRC.

Kwa wiki za hivi karibuni, maambukizi yameripotiwa pia katika nchi Jirani za Kenya, Nigeria na Uganda.

Kwa upande wake, Umoja wa Mataifa [UN] unayataja maambukizi ya sasa kuwa ni ya 17 katika historia ya DRC.

Related articles

Recent articles