15 C
New York

Mawaziri wapelekwa kambi ya jeshi

Published:

ADDIS ABABA, Ethiopia

WAZIRI Mkuu wa Ethiopia, Abiy Ahmed, amewapeleka mawaziri wake na baadhi ya vigogo wa serikali katika mafunzo ya kijeshi, akisema yatawasaidia kuimarisha uzalendo katika utumishi wa umma.

Katika picha aliyoposti mitandaoni, Abiy anaonekana akifanya mazoezi ya kijeshi na mawaziri, manaibu Waziri na viongozi wengine wa taasisi za serikali.

Miongoni mwa vigogo walioshiriki mazoezi hayo ni Spika wa Bunge, Muferiat Kamil, Waziri wa Fedha, Fitsum Assefa, na Waziri wa Afya, Mekdes Daba.

Kwa upande mwingine, hakuna taarifa zilizothibitisha siku rasmi mazoezi yalipoanza na ukomo wake.

Abiy ameyaita mazoezi hayo kuwa ni maalumu kwa ajili ya kuimarisha uzalendo kwa masilahi mapana ya maendeleo ya Ethiopia.

Related articles

Recent articles