13.9 C
New York

Simba yaliamsha dude tena, yaikanyaga Fountain Gate

Published:

Na mwandishi wetu, Gazetini

SIMBA ikiwa ugenini leo Oktoba 29, 2026, imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Fountain Gate, mfungaji wake akiwa ni beki wa kati wa kimataifa wa Afrika Kusini, Rushine De Reuck.

Vijana hao wa kocha Steven Barker walirejea dimbani wakiwa na ‘mzuka’ baada ya ushindi wa mabao 3-0 walioupata katika mchezo uliopita dhidi ya 15 de Agosto ya Guinea ya Ikweta.

De Reuck alifunga bao hilo katika dakika ya 34 ya kipindi cha kwanza, ukiwa ni mchezo wat isa kwa Simba tangu msimu huu wa Ligi Kuu Bara ulipoanza.

Kwa matokeo hayo, Wekundu wa Msimbazi wamebaki kileleni mwa msimamo wa Ligi, wakiwa na pointi 27, Yanga wakifuata katika nafasi ya pili wakiwa na pointi 22.

Related articles

Recent articles