MANCHESTER, Uingereza
LEJENDARI wa Manchester United, Gary Neville, amewataja Angel Di Maria na Antony kuwa ndiyo wachezaji wabovu zaidi kuwahi kusajiliwa na klabu hiyo tangu kocha Alex Ferguson alipoondoka.
Hii si mara ya kwanza kwa Neville kutoa maoni ya kuponda baadhi ya wachezaji na hata makocha waliowahi kuajiriwa tangu Ferguson alipoondoka.
Ferguson aliondoka Man United miaka 13 iliyopita na tangu hapo klabu hiyo imesajili wachezaji wengi, ingawa Neville anaamini Di Maria na Antony ndiyo ‘waliozingua’ zaidi.
“Di Maria alikuwa hovyo zaidi, ingawa nilivutiwa naye [aliposajiliwa]. Naweza kusema Antony na Di Maria. Silengi kumkosoa Antony lakini naye hakufanya lolote licha ya United kulipa fedha nyingi,” amesema Neville.
Di Maria alisajiliwa na Man United akitokea Real Madrid mwaka 2014, wakati Antony alijiunga na timu hiyo mwaka 2022 akitokea Ajax ya Uholanzi.


