14.4 C
New York

Haaland aweka mbili kuibeba Norway

Published:

OSLO, Norway

STRAIKA wa timu ya Taifa ya Norway, Erling Haaland, amefunga mabao mawili na kuliwezesha chama lake kupata ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya Denmark katika mchezo wa Ligi ya Mataifa ya Ulaya [Nations League] wa jana Septemba 24, 206.

Haaland anayekipiga Manchester City ni kama ameendeleza kiwango alichokuwa nacho kwenye fainali za Kombe la Dunia zilizopita, ambapo alimaliza akiwa amezifumania nyavu mara saba.

Katika mchezo dhidi ya Denmark, alifunga bao la kwanza kupitia ‘asisti’ ya winga Antonio Nusa. Alipachika la pili katika dakika ya 74.

Nyota wa zamani wa Man City anayekipiga Fulham kwa sasa, Oscar Bobb, naye aliifungia Norway akitumia asiti ya nahodha wa Arsenal, Martin Odegaard.

Kwa upande wa Denmark, mabao yao yalifungwa na kiungo wa Brentford, Mikkel Damsgaard, kwa shuti kali la nje ya boksi na straika wa zamani wa Manchester United, Rasmus Hojlund.

Related articles

Recent articles