18.6 C
New York

Huyu Raphinha ni moto wa kuotea mbali

Published:

CATALUNYA, Hispania

MSHAMBULIAJI wa Barcelona, Raphinha, amefunga ‘hat-trick’ yake ya pili katika michezo miwili mfululizo, safari hii akifnya hivyo dhidi ya Sevilla.

Barcelona wakiwa ugenini kwenye Uwanja wa Ramon Sanchez-Pizjuan, walipata ushindi wa mabao 3-1, ambapo alifunga katika dakika ya 22, 52 na 69 ya mchezo huo wa La Liga.

Raphinha raia wa Brazil, amefikisha mabao 14 katika mechi za mashindano mbalimbali aliyocheza msimu huu.

Kabla ya kukutana na Sevilla, Raphinha alifunga tena ‘hat-trick’ katika ushindi wa mabao 7-2 dhidi ya Racing Santander.

Kwa ushindi huo dhidi ya Sevilla, Barcelona imefikisha pointi 21 na kukaa kileleni mwa msimamo wa La Liga, ikiizidi sita Real Madrid inayoshika nafasi ya pili.

Related articles

Recent articles