18.6 C
New York

Pamba Jiji, Namungo kiboko kwa kugawa pointi

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

HOI kabisa! Kufikia hatua hii ya msimu wa 2026-27 wa Ligi Kuu Bara, Pamba Jiji na Namungo ndizo zinazoongoza kwa kufungwa mechi nyingi, hiyo ikiashiria hali mbaya na hata uwezekano wa kushuka daraja.

Iko hivi; Pamba Jiji inayoburuza mkia, imepoteza mechi tano kati ya sita ilizocheza, kama ilivyo Namungo ambayo hata hivyo imeshashuka dimbani mara saba.

Katika mechi zao sita, Pamba ya Mwanza haijabahatika kuonja ushindi, na badala yake imefungwa tano na kuambulia sare moja, hivyo kukaa mkiani ikiwa na pointi moja pekee.

Kwa upande wao, Namungo ya Wilayani Luangwa mkoani Lindi iko nafasi ya 13 kwenye msimamo huo wa timu 16 baada ya kukusanya pointi sita kwa kushinda mechi mbili na kufungwa tano.

Pamba imefunga mabao manne pekee na kuruhusu 13 katika mechi sita, wakati Namungo wenye michezo saba wamepasia nyavu mara sita na kuruhusu mabao 11.

Related articles

Recent articles