18.6 C
New York

Timu hizi ‘ukuta’ mbovu Ligi Kuu Bara 2026-27

Published:

Na Hassan Mwasha, Gazetini

KAZI ipo! Kagera Sugar ndiyo timu iliyoruhusu mabao mengi hadi sasa, ikiwa imecheza mechi sita msimu huu wa Ligi Kuu Bara [2026-27].

Katika michezo yao hiyo, Kagera Sugar imeruhusu nyavu zake kutikiswa mara 14, sawa na wastani wa mabao mawili kila mechi.

Ukiacha Kagera iliyo nafasi ya 15 kwenye msimamo, timu nyingine yenye mabao mengi ya kufungwa ni Pamba Jiji inayoburuza mkia ikiwa imefungwa mabao 13 katika mechi sita.

Timu zingine kwenye mwenendo huo ni Namungo [11], JKT Tanzania [10], Fountain Gate, Singida Black Stars na Coastal Union [9].

Kuziweka sawa takwimu, ukiacha Yanga na Simba [2] na Mbeya City na Dodoma Jiji [4], timu zote 12 zilizobaki zina wastani wa kuruhusu bao moja au zaidi katika kila mechi.

Related articles

Recent articles