LONDON, Uingereza
KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, amedai kuwa hajui lolote kuhusu kusaini mkataba mpya klabuni hapo.
Arteta raia wa Hispania aliyewahi kucheza eneo la kiungo katika kikosi cha Arsenal na timu ya Taifa ya Hispania, ameingia mwaka wa mwisho wa mkataba wake na klabu hiyo.
“Tumejipanga sana. Muda mwafaka ukifika, kila kitu kitawekwa wazi. Hakuna haja ya kuwa na wasiwasi,” amesema Mhispania huyo.
Kama itakumbukwa, Arteta alisainishwa mkataba mpya kipindi kama hiki mwaka 2024 na zipo taarifa kuwa kwa sasa kuna mazungumzo yanayoendelea.
Hata hivyo, Arteta ameweka wazi matamanio yake ya kubaki kwenye benchi la Washika Bunduki kwa miaka mingi ijayo.


