24.8 C
New York

Mbappe awataja ‘CR7’, Zidane

Published:

MADRID, Hispania

STAA wa Real Madrid, Kylian Mbappe, amesema Cristiano Ronaldo ‘CR7’, Zinedine Zidane na Ronaldo Nazario ni wachezaji ambao angeweza kuwasajili hata leo hii.

Nyota watatu hao waliwahi kupita Madrid na Ronaldo anaendelea kuwa mchezaji aliyefunga mabao mengi Zaidi katika historia ya klabuni hapo.

Katika maisha yake Santiago Bernabeu, Mreno huyo alifunga mabao 450 na kutwaa tuzo nne za Mchezaji Bora ya Ballon d’Or.

Nazario alibeba Ballon d’Or moja, pia akitwaa mataji mawili ya Ligi Kuu [La Liga], wakati Zidane naye alibeba tuzo hiyo na kuwa kocha baadaye klabuni hapo.

Mbappe alijiunga na Madrid miaka mitatu iliyopita na tayari ameshazipasia nyavu mara 100 kwa kipindi alichodumu kwenye klabu hiyo.

Kwa misimu yake miwili Bernabeu, Mbappe alifunga mabao 86, pia akibeba mfululizo tuzo ya mfungaji bora wa Ligi.

Related articles

Recent articles