RIO, Brazil
MKONGWE wa soka la Brazil, Marcelo, amemchagua tena Cristiano Ronaldo alipoulizwa ni nani mkali wa muda wote kati ya Mreno huyo na Lionel Messi.
Inafahamika kuwa Marcelo na Ronaldo walikuwa pamoja kwa miaka tisa wakiwa kwenye kikosi cha Real Madrid.
Hii si mara ya kwanza kwa Marcelo kumtaja Ronaldo mbele ya Messi kwani aliwahi kufanya hivyo Desemba, 2025.
“Tuna bahati sana kuwashuhudia wote. Hatukuwaona Pele na Maradona lakini tumewaona Cristiano na Messi. Navutiwa zaidi na Cristiano …” amesema Marcelo.
Marcelo ameshastaafu kandanda lakini Messi na Ronaldo bado wanaendelea kuupiga. Mreno huyo yuko Saudi Arabia, wakati Messi anakipiga Marekani.


