24.8 C
New York

Carrick afunguka kufukuzwa Man United

Published:

MANCHESTER, Uingereza

KOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amefunguka juu ya tetesi zinazodai kuwa mabosi wa klabu hiyo watamfungashia virago.

Taarifa zilizopo, ambazo hata hivyo hazijathibitishwa na uongozi wa Man United, zinadai kuwa atafukuzwa endapo timu hiyo itapoteza mechi ya Jumapili hii dhidi ya Fulham.

Man United imepoteza mechi mbili zilizopita, zote za nyumbani, ambapo ilifungwa na Manchester City na Brighton & Hove Albion.

Akizungumzia tetesi za kufutwa kazi, Carrick amesema: “Nadhani bado nina muda wa zaidi ya matokeo ya mechi mbili.

Katika hatua nyingine, kiungo huyo wa zamani amekiri kuwa anapaswa kubeba lawama juu ya kiwango kibovu cha timu hiyo msimu huu.

Related articles

Recent articles