25.7 C
New York

Baada ya sare, Carrick alia na wachezaji

Published:

MANCHESTER, Uingereza

KOCHA wa Manchester United, Michael Carrick, amesema kiwango kibovu kilichooneshwa na wachezaji wake kilichangia matokeo ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya Everton jana Septemba 6, 2026.

Kwa matokeo hayo, sasa Man United imefikisha mechi tatu za Ligi bila ushindi tangu msimu huu wa 2026-27 ulipoanza.

Dhidi ya Everton, Man United ilionekana kuwa na uhakika wa pointi tatu ikiongoza kwa mabao 2-1, kabla ya bao la Ainsley Maitland-Niles kuipa sare Everton.

Akizungumzia mchezo huo, Carrick amesema vijana wake waliuanza kwa kiwango bora, lakini Kadiri muda ulivyosogea, walianza kupoteana.

“Kwa sehemu kubwa, tulijilinda vizuri kama timu. Muda ulivyoendelea kusogea, tuliianza kuacha kufanya maamuzi sahihi …” amesema.

Related articles

Recent articles