25.7 C
New York

Mbappe ajitabiria Ballon d’Or

Published:

MADRID, Hispania

MSHAMBULIAJI wa Real Madrid, Kylian Mbappe, anaamini huu ni mwaka wake wa kuitwaa kwa mara ya kwanza tuzo maarufu ya Ballon d’Or.

Hafla ya kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo kwa mwaka huu inatarajiwa kufanyika Oktoba 26, 2026.

Mfaransa huyo mwenye umri wa miaka 27, alimaliza msimu uliopita (2025-26) akiwa amefunga mabao 42 katika michezo 44 ya mashindano mbalimbali, ingawa Madrid haikutwaa taji lolote.

Hata hivyo, aliibeba tuzo ya mfungaji bora katika fainali za Kombe la Dunia akiwa amezipasia nyavu mara 10, akifikisha mabao 22 kwenye historia ya michuano hiyo.

“Nafikiri inapocheza Real Madrid, klabu bora zaidi duniani, watu wanakuhusisha na tuzo hii. Wengi wananizungumzia kuhusu Ballon d’Or,” amesema.

Mara ya mwisho kwa Mbappe kushika nafasi za juu kwenye kinyang’anyiro cha tuzo hiyo ilikuwa mwaka 2023, ambapo alikuwa wa tatu wakati huo akikipiga PSG.

Mbappe anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa straika wa Bayern Munich na nahodha wa timu ya soka ya Taifa ya England, Harry Kane.

Msimu uliopita, Kane aliifungia Bayern jumla ya mabao 61 katika mechi 51 na kuiwezesha timu hiyo ya Ujerumani kutwaa mataji mawili. Alifunga mara sita katika fainali zilizopita za Kombe la Dunia.

Related articles

Recent articles