LOS ANGELES, Marekani
BIBIYE mwenye jina kubwa katika soko la muziki nchini Marekani, Ciara, ametangaza kuwa ana ujauzito, hivyo mtoto ajaye atakuwa wa tano kwenye familia yake na mumewe, Russell Wilson.
Ciara ameweka wazi hilo jana Septemba 6, 2026, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram.
Itakumbukwa kuwa Ciara aliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi na rapa Bow Wow kuanzia mwaka 2004 lakini waliachana miaka miwili tu baadaye.
Mwaka 2013, alivishwa pete ya uchumba na rapa mwingine, Future, ambaye walibahatika kupata mtoto mmoja wa kiume mwaka uliofuata, kisha kuachana.
Alianza mahusiano na Wilson mwanzoni mwa mwaka 2015 na kufunga ndoa Julai 6, 2016. Wawili hao wana watoto watatu waliozaliwa mwaka 2017, 2020 na 2023.


