20.4 C
New York

Trump: Tunakwenda ‘kuipelekea moto’ zaidi Iran

Published:

WASHINGTON DC, Marekani

RAIS wa Marekani, Donald Trump, amesema wanajeshi wake watafanya mashambulizi makali dhidi ya Iran baada ya kile walichokifanya wenzao hao.

Hivi karibuni, Iran ilishambulia kambi ya kijeshi nchini Jordan, jambo ambalo Rais Trump amesema hawatolifumbia macho. “Tunakwenda kuwashambulia kwa uzito wa juu,” amesema.

Kwa upande wake, jeshi la Iran (IRGC) limedai kuwa mifumo yake ya anga imenasa na kuisambaratisha ndege isiyo na rubani ya Marekani aina ya MQ-9.

Aidha, Iran ilikiri kufanya shambulizi huko Jordan, ikidai kuwa ililipiza kisasi baada ya Marekani kushambulia meli zake mbili katika Mlango-Bahari wa Hormuz.

Katika hatua nyingine, Rais Trump ameeendelea kusisitiza kuwa kwa sasa hali ni shwari katika Mlango-Bahari wa Hormuz.

Related articles

Recent articles