23.5 C
New York

Watatu waomba kuondoka Tottenham

Published:

LONDON, Uingereza

KOCHA wa Tottenham, Roberto De Zerbi, amefichua kuwa mastaa wake watatu kikosini wameomba kuondoka klabuni hapo.

Zerbi raia wa Italia, ameenda mbali zaidi na kuwataja nyota hao kuwa ni Richarlison, Kevin Danso na Pape Matar Sarr.

Kwa pamoja, wachezaji wote hao hawakuwa kikosini wakati Tottenham ilipofungwa mabao 2-0 na Newcastle United jana Agosti 29, 2026.

Awali, Sunderland ilifika mezani na ofa ya kumtaka beki wa kati, Danso, lakini ilikataa kupokea ofa hiyo. Juventus wao wanamtaka Sarr.

Akimzungumzia Richarlison, De Zerbi alisema: “Kwa Richarlison sijajua. Alisema mara nyingi tu, kwamba anataka kuondoka.”

Related articles

Recent articles