MANCHESTER, Uingereza
KLABU ya Manchester City imeanza mazungumzo na Liverpool ikijaribu kuishawishi iwauzie winga raia wa Ureno, Cody Gakpo.
Man City imechukua hatua huku dirisha kubwa la usajili wa kiangazi likitarajiwa kufungwa Jumanne ya wiki ijayo.
Taarifa za Gakpo kuondoka zinakuja wakati huu Liverpool wakitajwa kukaribia kumsajili mshambuliaji kutoka PSG, Bradley Barcola, kwa Pauni milioni 123.
Katika hatua nyingine, kinda wa Manchester United, James Scanlon, amejiunga na Washika Bunduki wa London, Arsenal.
Scanlon mwenye umri wa miaka 19, alishindwa kuwika Man United, ambapo msimu uliopita alicheza kwa mkopo
Swindon Town. Alifunga bao moja katika mechi sita.


