23.9 C
New York

Man United yamnasa Baleba

Published:

MANCHESTER, Uingereza

KLABU ya Manchester United imekamilisha usajili wa kiungo wa kimataifa wa Cameroon, Carlos Baleba baada ya kukubali ada ya Pauni milioni 70.

Kwa mujibu wa ripoti, Man United wameitangulizia Brighton kiasi cha Pauni milioni 65 kumnasa nyota huyo mwenye umri wa miaka 22.

Man United wameboresha eneo la kiungo kwa kuwasajili Andrey Santos kutoka Chelsea na Youri Tielemans aliyekuwa Aston Villa.

Ripoti zinaeleza kuwa Baleba amesaini mkataba wa miaka mitano kuitumikia miamba hiyo ya Old Trafford na ataongezwa miezi 12 endapo watavutiwa na uwezo wake.

“Ni jambo zuri sana kujiunga na klabu ya ndoto zangu. Kucheza Old Trafford ni jambo la pekee na kuwa mchezaji wa Manchester United ni furaha iliyoje,” amesema Baleba.

Baleba, ambaye alijiunga na Brighton mwaka 2023 akitokea Lille, kwa sasa anauguza majeraha ya goti aliyopata akiwa kwenye kambi ya ‘pre-season’ nchini Austria.

Kwa miaka takribani mitatu aliyocheza Brighton, ametumika katika michezo 112, akifunga mabao nane. Alicheza mechi 31 za Ligi Kuu msimu uliopita (2025-26).

Related articles

Recent articles