23.7 C
New York

Barca yampa Rodri jezi namba 16

Published:

CATALUNYA, Hispania

KIUNGO wa kimataifa wa Hispania aliyejiunga na Barcelona akitokea Manchester City, Rodri, amepewa jezi namba 16 katika kikosi cha Wacatalunya hao.

Aliyefichua hayo si mwingine, bali ni mwandishi wa habari maarufu wa Italia, Fabrizio Romano, kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X.

“Rodri alizungumza na Fermin Lopez na kumuomba amwachie jezi namba 16 ,” amesema Romano, ambaye anasifika kwa ukweli wa taarifa zake za usajili.

Katika hatua nyingine, Romano amefichua kuwa Lopez amechagua kutumia jezi namba 7. Rodri atasaini mkataba wa miaka minne wiki hii, ambao utambaliza Camp Nou hadi Juni, 2030.

Kama itakumbukwa, Rodri aliyewahi kutwaa tuzo ya Ballon d’Or, hakuwa sehemu ya kikosi cha Man City kilichofangwa mabao 3-0 na Arsenal katika mchezo wa juzikati wa Ngao ya Jamii.

Related articles

Recent articles