MILAN, Italia
KUMEKUCHA! Mechi ya kwanza ya Ligi Kuu ya Italia (Serie A) kwa msimu wa 2026-27 itachezwa Agosti 17, 2026, ambapo Udinese itavaana na Como.
Inter Milan ya kocha Christian Chivu inaingia msimu mpya ikiwa bingwa mtetezi baada ya taji la Serie A ililobeba kwa tofauti ya pointi 17.
Napoli, AC Milan, Atalanta na Lazio, kila moja imefumua benchi la ufundi na kuajiri kocha mpya. Milan imempa ajira kocha wa zamani wa Manchester United, Ruben Amorim, wakati Napoli imemchukua mkongwe Max Allegri.
Wakati huo huo, Juventus na Milan zina hasira baada ya kushindwa kumaliza ndani ya ‘Top Four’ msimu uliopita (2025-26).
Aidha, Como inayonolewa na kiungo wa zamani wa Arsenal na timu ya Taifa ya Hispania, Cesc Fabregas, nayo si ya kupuuzwa. Ilimaliza msimu uliopita ikiwa na tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa (2026-27).
Je, Fabregas atarudi alichokifanya msimu uliopita au atapotea? Roma nayo si ya kuiweka kando kwenye vita ya ubingwa au ndani ya nafasi nne za juu.
Roma ambayo haijatwaa ubingwa wa Ligi Kuu tangu mwaka 2001, inanolewa na kocha Gian Piero Gasperini na ilimaliza msimu uliopita (2025-26) ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo wa Serie A.


