30 C
New York

Hizi ndizo nchi zinazoendeleza hukumu ya kifo

Published:

BEIRUT, Lebanon

LEBANON imekuwa nchi ya kwanza ya Mashariki ya Kati kufuta sheria ya hukumu ya kifo kwa wafungwa wake. Hatua hiyo ilifikiwa hivi karibuni baada wabunge 128 wa Taifa hilo kupiga kura ya kuikataa adhabu hiyo.

Badala ya kunyongwa kama ilivyokuwa awali, sasa hukumu kali zaidi itakuwa kifungo cha maisha na kazi ngumu gerezani.

Kufikia mwishoni mwa mwaka 2025, wafungwa 85 walikuwa wakisubiri hukumu ya kifo, kwa mujibu wa ripoti ya mamlaka za Lebanon.

Katika ripoti yake, Shirika la Haki za Binadamu la Amnesty International linaeleza kuwa takribani robo tatu ya nchi duniani zilishaachana na hukumu ya kifo kufikia Desemba, 2025.

Kwamba katika nchi hizo, hakuna mfungwa aliyenyongwa kwa kipindi cha miaka 10 ya hivi karibuni.

Hata hivyo, takwimu za Amnesty International zinaonesha kuwa kwa mwaka 2025, wafungwa 2,707 walinyongwa, likiwa ni ongezeko la asilimia 78, ikilinganishwa na 1,518 kwa mwaka 2024.

Shirika hilo linaitaja Iran kuwa ndiyo nchi iliyoongoza duniani kwa idadi kubwa ya wafungwa walinyongwa mwaka 2025, ambao ni 2,159, ikilinganishwa na 972 kwa mwaka 2024.

Kwa upande mwingine, Amnesty International wanatilia shaka kuwa huenda China ina idadi kubwa pia, ingawa imekuwa ikificha idadi halisi ya wafungwa walionyongwa.

Related articles

Recent articles