DAMASCUS, Syria
MAHAKAMA Kuu ya Syria imemuhukumu kifo aliyekuwa Rais wa Taifa hilo, Bashar al-Assad, baada ya kumkuta na hatia katika mashitaka ya uhalifu dhidi ya binadamu wakati wa vita vya wenyewe kwa wenyewe.
Assad ameshukiwa na hukumu hiyo akiwa hayuko Syria kwani amekuwa akiishi na familia yake nchini Urusi tangu utawala wake wa 21 ulipoangushwa Desemba, 2024.
Hukumu ya kifo imemkuta pia binadamu yake, Atef Najib, ambaye alikuwa kiongozi wa usalama huko Kusini mwa Syria katika Jimbo la Deraa.
Deraa ndiko yalikoanzia maandamano ya kupinga utawala wa kidikteta wa Assad. Hasira za wananchi zilianza Machi, 2021, baada ya mamlaka kuwakamata na kuwatesa baadhi ya vijana waliotajwa kuandika jumbe za kuikosoa Serikali.
Baadaye, maandamano hayo yalisambaa nchini nzima na kusababisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyogharimu maisha ya maelfu ya raia
Kwa upande wake, Najib aliyekuwa akiishi Syria, alikuwa mahakamani wakati hukumu hiyo ikisomwa, akiwa amevalia sare za wafungwa.
Najib alishitakiwa kwa uhalifu dhidi ya binadamu, yakiwamo mauaji ya watoto wenye umri chini ya miaka 15.
Ndugu mwingine wa Assad aliyekumbana na hukumu ya kifo ni mdogo wake, Maher, ambaye naye amekuwa akiishi Moscow, Urusi. Alikuwa kiongozi wa jeshi wakati wa uongozi wa Assad.
Wakati huo huo, aliyekuwa Waziri wa Ulinzi, Fahd al-Freij, naye ameingia kwenye kitanzi kilichowavaa Assad, Najib na Maher.
Je, Urusi itawakamata Assad na Maher na kuwakabidhi kwa Syria ili wakatumikie hukumu zao?
Kwa sasa, Syria iko chini ya Rais Ahmed al-Sharaa, ambaye aliliongoza jeshi kumtoa madarakani Assad baada ya kuona wananchi ‘wamekomaa’ wakitaka ajiuzulu.
Tangu alipoingia madarakani miaka mitano iliyopita, al-Sharaa amesimamia kukamatwa kwa baadhi ya vigogo wa Serikali iliyokuwa ikiongozwa na Assad.
Assad aliingia madarakani mwaka 2000 baada ya kifo cha baba yake, Hafez al-Assad. Akiwa mtoto wa pili wa kiume, alipata nafasi ya uongozi kwa kuwa kaka yake, Basil, alifariki kwa ajali ya gari mwaka 1994.
Usikose sehemu ya pili ya makala haya … Tembelea www.gazetini.co.tz


