4.8 C
New York

Diwani awapiga ‘jeki’ walimu waliong’ara darasa la saba

Published:

Na Editha William, Gazetini- KAGERA

DIWANI wa Kata ya Ibwera, Ashiraf Nyangasha, ametimiza ahadi yake kwa kutoa zawadi ya Shilingi 2,743,000 kwa walimu waliofanya vizuri katika matokeo ya mtihani wa kuhitimu Darasa la Saba, ikiwa ni sehemu ya kutambua na kuhamasisha juhudi zao katika kuinua kiwango cha elimu.

Zawadi hiyo imetolewa leo Novemba 13, 2026, katika hafla iliyofanyika Sunrise Beach, Manispaa ya Bukoba, ikiwakutanisha walimu kutoka shule zote za msingi na sekondari, wakiongozwa na Mtendaji wa Kata na Afisa Elimu Kata, pamoja na maafisa mbalimbali wa Kata ya Ibwera.

Katika matokeo ya mwaka huu, Kata ya Ibwera imefanikiwa kushika nafasi ya pili kati ya kata 29 za Halmashauri ya Bukoba.

Akizungumza katika hafla hiyo, Nyangasha amesema katika kipindi chake cha kwanza cha udiwani aliikuta Kata ya Ibwera ikiwa miongoni mwa kata zilizokuwa zikifanya vibaya katika matokeo ya kitaaluma.

“Niliamua kuchukua hatua kwa kufanya ziara katika kila shule, kukutanisha walimu na wazazi, pamoja na kuweka mikakati na motisha kwa walimu ili kuboresha ufaulu na jitihada hizo zimeanza kuzaa matunda,”

Nyangasha amesisitiza kuwa walimu ni msingi muhimu katika maendeleo ya jamii na hawezi kuona wakitumika katika shughuli mbalimbali, kisha kusahaulika baada ya kumaliza majukumu yao.

Akiwa sehemu ya waliohudhuria hafla hiyo, Katibu Tawala wa Wilaya ya Bukoba, Proscovia Jaka Mwambi, aliwapongeza walimu kwa kazi nzuri wanayoifanya na kuwataka kutambua umuhimu wao kwenye sekta ya elimu na jamii kwa ujumla.

Related articles

Recent articles