MANCHESTER, Uingereza
BAADA ya kufukuzwa Manchester United, Michael Carrick amewaaga kwa barua yenye ujumbe mzito mashabiki wa klabu hiyo.
Carrick ameichapisha mitandaoni barua hiyo muda mfupi baada ya Man United kumtangaza Mauricio Pochettino kuwa kocha wao mpya.
Katika barua yake, kocha huyo mwenye umri wa miaka 45 amewashukuru mashabiki na wafanyakazi wa klabu hiyo kwa kuwa naye bega kwa bega kwa kipindi chote alichodumu kwenye benchi la ufundi.
“Wapendwa mashabiki wa United. Ilikuwa ni heshima kubwa kwangu kuinoa Manchester United, klabu ninayoipenda.
Aidha, katika barua yake, amewashukuru wasaidizi wake wa benchi la ufundi, akisema walisimama naye hata pale mambo yalivyoonekana kwenda vibaya.
Wakati huo huo, Carrick amekiri kuwa ataendelea kuwa sehemu ya familia ya Man United, ikiwamo kufuatilia mechi na hata kushangilia pale inapopata matokeo mazuri ndani ya uwanja.


