4.8 C
New York

Wachezaji wa kigeni wazua jambo Muhaj Cup 2026

Published:

Na Editha William, Gazetini – KAGERA

ACHANA na matokeo ya mchezo wa jana Novemba 11, 2026, uliozikutanisha Kashabo FC na Mchikichini FC katika michuano ya Muhaj Cup 2026 inayoendelea katika Kata ya Hamgembe, Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera.

Moja ya timu zinazoshiriki Ligi hiyo ya timu nne kutoka Kata hiyo, Omukishenye FC, imeibua madai ya baadhi ya wapinzani wao kutumia wachezaji wasiokuwa wazawa na wakazi wa Hamgembe.

Baadhi ya wachezaji wa Omukishenye FC na mashabiki wameibua mjadala huo, huku baadhi ya wadau wa soka wakisisitiza umuhimu wa kuzingatia malengo ya msingi ya kuanzishwa kwa michuano hiyo.

“Muhaj Cup 2026 ni mashindano yanayolenga kuzikutanisha timu za ndani ya Kata kwa lengo la kuibua na kupata kikosi kimoja bora kitakachoiwakilisha Kata nzima ya Hamgembe,” amesema mmoja ya wadau hao.

Katika mchezo huo wa kwanza kwa kila timu, Kashabo FC iliondoka na pointi tatu kwa ushidi wa mabao 2-1 dhidi ya wenzao wa Mchikichini FC, licha ya kiwango kizuri kilichooneshwa na timu zote mbili kwa dakika zote 90.

Related articles

Recent articles