21 C
New York

Visual| TB bado ni janga nchini

Published:

Pamoja na nguvu kubwa ambayo imekuwa ikitumika na Serikali ya Tanzania katika kutokomeza Kifua Kikuu lakini takwimu zinaonyesha kwamba bado kuna kazi kubwa ya kufanya ili kuukabili ugonjwa huo.

Kwani kwa mujibu wa Ripoti ya Shirika la Afya Duniani(WHO), Tanzania ni miongoni mwa nchi 30 zenye maambukizi makubwa ya ugonjwa wa TB zinazochangia asilimia 87 ya wagonjwa wote duniani.

Ripoti hiyo ya WHO inaongeza kuwa kwa mwaka 2019 peke kulikuwa na wagojwa wapya wa TB milioni 10 duniani ambao kati yao milioni 1.4 sawa na asilimia 14 walifariki dunia.

Upande wa Tanzania mwaka 2019 ilikuwa na wagonjwa wapya wa TB 137,000 ambapo kati ya hao wagonjwa 82,166 sawa na asilimia 59 waligundulika na kupatiwa matibabu.

Changamoto ya Kifua Kikuu au TB ni kubwa kwani inachangia kuongeza vifo nchini kwa watu wenye wagonjwa mengine. Tafiti zinaonyesha kwamba zaidi ya asilimia 44 ya vifo vya watu wanaoishi na Virusi Vya UKIMWI (WAVIU) husababishwa na TB.

Aidha, Kamati ya Kudumu ya  Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI ya mwaka ya Shughuli zilizotekelezwa kwa kipindi cha Januari 2021 hadi Januari 2022 inabainisha kuwa, takwimu hizo zinazidhihirisha ya kuwa TB bado ni janga la Kitaifa.

“Takwimu hizi zinadhihirisha ya kuwa TB bado ni janga la kitaifa hapa nchini mwetu kama ilivyo pia janga la kidunia tangu ilipotangazwa hivyo mwaka 1993. Aidha Kamati imebaini upungufu wa mashine za Gene-Xpert ambazo hutumika kupimia ugunduzi wa TB,”inaeleza Ripoti hiyo ya Kamati.

Pia Kamati hiyo ya bunge imeshauri mbinu zinazoweza kutumika katika kupambana na TB nchini ikiwa ni pamoja na maboresho ya huduma ikiwamo vifaa na utoaji elimu kwa watumishi na jamii kwa ujumla.

“Serikali kuendelea kuboresha huduma za ugunduzi wa TB kwa kupanua teknolojia mpya ya vinasaba ya Gene Xpert inayotoa majibu kwa haraka ndani ya saa mbili na mashine za hadubini ambazo hutoa majibu baada ya saa 48 katika Halmashauri zote nchini na kuimarisha mfumo wa usafirishaji wa sampuli kwa vituo vilivyo mbali na maabara ili kuhakikisha kila mhisiwa wa TB anafanyiwa uchunguzi.

“Aidha, kuhakikisha halmashauri zote zinatekeleza mfumo wa uchunguzi na ugunduzi wa TB katika vituo vyetu ulioboreshwa “Quality Improvement in TB case detection” katika vituo vya kutolea huduma za afya,” inabainisha ripoti hiyo.


Pia inaendelea kushauri kuwa serikali iendelee kutoa elimu kwa jamii kuhusu athari na
dalili za TB na Ukoma na namna ya kukabiliana na magonjwa haya kwa kupitia redio, televisheni, vipeperushi, Tovuti na mitandao ya kijamii (facebook, tweeter na Instagram).

“Aidha Wizara iwajengee uwezo watoa huduma za TB ngazi ya jamii ikiwepo vikundi vya wagonjwa
waliowahi kuugua TB na kupona (Ex-TB patient) katika halmashauri zote nchini ili waweze kutoa elimu, kuhamasisha jamii, kusimamia matibabu nyumbani na kutoa rufaa kwa walio na dalili kwenda kwenye vipimo.

“Kamati inasisitiza kwamba Serikali iendelee kutekeleza kampeni mbalimbali za uhamasishaji na upimaji wa TB na VVU kwa wananchi katika makazi duni yenye msongamano au sehemu za kazi zenye mazingira hatarishi kama vile maeneo ya migodi, magerezani na makazi duni, miji mikubwa na shule za bweni.

“Vileviled, Kampeni maalumu zifanyike katika vijiji vyote vyenye idadi ya wagonjwa wengi wa Ukoma. Kampeni hii ihusishe pia kufanya ufuatiliaji wa kaya zenye wagonjwa na watu wao wa karibu (contact tracing) na kutoa tiba kinga,” imebainisha ripoti hiyo ya Kamati.

Ni wajibu pia wa wananchi kuhakikisha kuwa wanafika katika vituo mbalimbali vya afya ambavyo vinatoa huduma ya uchunguzi wa kifua kikuu au TB pale wanapokooa mfululizo.

Kwani hii siyo tu kwamba itasaidia kujua hali zao mapema lakini pia kuanza matibabu kwa wakati waipo watabainika kuwa na ugonjwa huo na hatimaye kuwa na taifa la watu wenye afya bora bila magonjwa.

Related articles

spot_img

Recent articles

spot_img