25.2 C
New York

Infantino anyoosha mikono, aachana na mpango wake

Published:

NYON, Uswis

HATIMAYE Rais wa Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Gianni Infantino, ametangaza kuachana na mpango wake wa kuuza hisa za Kombe la Dunia na michuano mingine ya Taasisi hiyo.

Awali, Infantino aliweka mikakati wa kuuza hisa kwa kampuni binafsi, lengo likiwa ni kutanua mapato ya mashindano yote makubwa yanayosimiwa na Shirikisho hilo.

Infantino alienda mbali zaidi na kuahidi kila mwanachama wa FIFA kupewa Dola milioni 40 endapo angeunga mkono mchakato huo.

Hata hivyo, mpango huo ulikosolewa vikali na wadau wa soka, wakiamini mashindano hayo yangepoteza uwezo wa kujisimamia na badala yake hata bingwa angepatikana kibiashara.

Miongoni mwa wakosoaji wakubwa ni Shirikisho la Soka la Ulaya (UEFA) lililoahidi kususia Kombe la Dunia endapo Infantino angeendelea na mpango wake huo.

Waziri Mkuu mpya wa Uingereza, Andy Burnham, alienda mbali zaidi na kusema Infantino si mtu sahihi kuiongoza taasisi kubwa kama FIFA.

Related articles

Recent articles