20.5 C
New York

Arteta asema msimu ujao wanabeba tena

Published:

LONDON, Uingereza

KOCHA wa Arsenal, Mikel Arteta, amewaahidi makubwa mashabiki wa timu hiyo, akisema watarajie tena ubingwa wa Ligi Kuu ya England (EPL).

Arsenal walimaliza msimu uliopita (2025-26) wakiwa mabingwa baada ya kuizidi pointi saba Manchester City iliyoshika nafasi ya pili.

“Lengo langu ni kuhakikisha tunaendelea kuwa bora zaidi na kufikia viwango tulivyoweka. Ndicho tunachopaswa kufanya,” amesema.

Arteta ndiye kocha wa muda mrefu zaidi, ikilinganishwa na wengine wote atakaowania nao ubingwa msimu ujao wa Ligi Kuu ya England (EPL).

Hata hivyo, klabu za Chelsea, Liverpool na Manchester City ziko chini ya makocha wapya, jambo linaloweza kuongeza ushindani zaidi.

Related articles

Recent articles