MANCHESTER, Uingereza
KOCHA wa zamani wa Manchester United, Ruben Amorim, amedai kuwa hapaswi kulaumiwa kwa kufeli kwake klabuni hapo.
Kwa mujibu wake, lawama zinapaswa kuelekezwa kwa wote, wakiwamo viongozi wa klabu hiyo ya jijini Manchester.
Akihojiwa na kituo cha televisheni cha Sky Italia, Mreno huyo amesema amejifunza mengi katika maisha yake pale Old Trafford.
Baada ya mwenendo usioridhisha wa timu hiyo, Amorim alifukuzwa Januari, 2026, na nafasi yake kuchukuliwa na Michael Carrick.
“Jambo la kwanza ni kwamba haijalishi tena. Ni hisia tu. Hiyo ni historia, huwa inatokea. Mazingira huwa yanabadilika. Tuangalie yajayo,” amesema.
Amorim, kocha wa zamani wa Sporting Lisbon, amerejea kazini na msimu ujao (2026-27) atakuwa kwenye benchi la ufundi la AC Milan.


