29 C
New York

Joshua amtwanga mtu kwa ‘KO’

Published:

RIYADH, Saudi Arabia

BONDIA wa ngumi za uzito wa juu, Anthony Joshua, amempiga kwa KO ya raundi ya pili Kristian Prenga, pambano lililopigwa mjini Jeddah, Saudi Arabia, usiku wa jana Julai 25, 2026.

Hayo ni maandalizi ya Joshua kumvaa mpinzani wake mkubwa, Tyson Fury, katika pambano linalotarajiwa kupigwa kabla ya mwaka huu kuisha.

Dhidi ya Prenga, Joshua alionesha dalili za kupotea baada ya kuangushwa katika raundi ya kwanza, kabla ya kuinuka na kuendelea.

Katika raundi ya pili, Muingereza huyo ambaye ni bingwa wa dunia mara mbili, alitumia dakika moja na sekunde 52 tu kummaliza mpinzani wake huyo.

Hivyo, pambano lao hilo lililosubiriwa kwa hamu na wapenzi wa ndondi ulimwenguni kote lilimalizika ndani ya dakika nne na sekunde 52 tu.

Related articles

Recent articles