29 C
New York

Di Maria ataka Messi asistaafu

Published:

LONDON, Uingereza

LEJENDARI wa timu ya soka ya Taifa ya Argentina, Angel Di Maria, amemtaka Lionel Messi kuachana na wazo la kutundika daluga.

Di Maria amekuja na ushauri huo zikiwa ni siku chache tu zimepita tangu Messi na Argentina walipopoteza Kombe la Dunia kwa kufungwa na Hispania katika mechi ya fainali.

Tangu kumalizika kwa michuano hiyo Julai 19, 2026, Messi mwenye umri wa miaka 39 ameonekana kujipanga kustaafu kuitumikia timu ya taifa.

Hata hivyo, Di Maria amemtaja nyota huyo kama mchezaji bora zaidi kuwahi kutokea katika historia ya mchezo wa kandanda.

Kwa mujibu wa Di Maria aliyewahi Manchester United na PSG, Messi bado ana muda mrefu wa kucheza timu ya taifa kwa miaka mingi zaidi.

“Ndiyo, Leo anapaswa kuendelea kucheza kwa muda wowote anaotaka. Nafikiri anaweza kuendelea kwa miaka mingi ijayo,” amesema Di Maria katika mahojiano yake na kituo cha televisheni cha TNT Sports.

Related articles

Recent articles