LONDON, Uingereza
WAKATI Alex Ferguson akiwa ndiye kocha aliyehudumu kwa muda mrefu mrefu Ligi Kuu ya England (EPL), Sam Allardyce naye ana historia yake kwenye michuano hiyo.
Iko hivi; Ferguson aliajiriwa na Manchester United mwaka 1986 hadi alipojiuzulu mwaka 2023 akiwa amefanya kazi siku 9,704.
Hata hivyo, Allardyce anabaki kuwa ndiye kocha aliyezinoa timu nyingi katika historia ya Ligi Kuu hiyo. Muingereza huyo amefanya kazi na klabu tisa tofauti.
Wanaofuatia ni Roy Hodgson na Mark Hughes, kila mmoja akiwa amefanya kazi katika mabenchi ya timu sita za EPL.
Pia, kuna makocha Steve Bruce, Harry Redknapp na Alan Pardew, ambao kila mmoja amezinoa timu tano.


