28 C
New York

Pirlo anukia ukocha Italia

Published:

MILAN, Italia

MKONGWE wa klabu ya AC Milan, Andrea Pirlo, anakaribia kutangazwa kuwa kocha mkuu wa timu ya soka ya Taifa ya Italia.

Kwa mujibu wa mwandishi wa habari maarufu wa Italia, Fabrizio Romano, Shirikisho la Soka nchini humo limeshawasiliana na Pirlo.

Ripoti zinaeleza kuwa Shirikisho limemgeukia Pirlo baada ya Pep Guardiola na Carlo Ancelotti kukataa ofa hiyo.

Italia haina kocha mkuu tangu Gennaro Gattuso alipoachana nayo baada ya kushindwa kufuzu fainali za Kombe la Dunia za mwaka huu (2026).

Hivi karibuni, taarifa zilidai kuwa Shirikisho limefanya mawasiliano na Guardiola ambaye amekuwa nje ya kazi tangu alipoondoka Manchester City mwishoni mwa msimu wa 2025-26.

Related articles

Recent articles