28 C
New York

Mkongwe Arsenal apata ulaji Ujerumani

Published:

MUNICH, Ujerumani

BEKI wa kati wa zamani wa Arsenal, Per Mertesacker, ameteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Michezo wa Chama cha Soka cha Ujerumani (DFB).

Mertesacker mwenye umri wa miaka 41, amepewa ajira hiyo akichukua nafasi ya Andreas Rettig na amesaini mkataba utakaokwisha mwaka 2030.

Kwa mujibu wa ripoti zilizothibitishwa na DFB, mlinzi huyo ataanza majukumu yake Januari Mosi, 2027.

Katika kibarua chake hicho, Mertesacker atasimamia timu ya wakubwa ya Ujerumani, pamoja na ‘academy’ yake.

Aidha, taarifa za kuajiriwa DFB zinakuja ikiwa ni miezi nane tu imepita tangu alipoondoka Arsenal, ambako alikuwa kocha wa timu za vijana.

Ujerumani imechukua hatua hiyo baada ya kumtangaza pia Jurgen Klopp kuwa kocha wake wa timu ya taifa.

Related articles

Recent articles