23.1 C
New York

Mastaa Argentina wamkataa Rais Trump

Published:

MIAMI, Marekani

NYOTA wawili wa timu ya soka ya Taifa ya Argentina, Lisandro Martinez na Cristian Romero, walionekana wakikwepa kupeana mikono na Rais wa Marekani, Donald Trump.

Ni wakati wa kukabidhiwa medali ya kufika fainali ya msimu huu wa Kombe la Dunia, ambapo Argentina walikosa ubingwa baada ya kufungwa bao 1-0.

Baada ya mchezo, kama ilivyo kawaida, mgeni rasmi, Rais Trump, alitakiwa kuwavalisha medali wachezaji wa timu zote, akianza na Argentina.

Baada ya Martinez ‘kupotezea’ mkono wa Rais Trump, Romero naye alifanya hivyo, kisha kuwasalimia Rais wa Mexico, Claudia Sheinbaum, na Waziri Mkuu wa Canada, Mark Carney.

Tukio hilo linakuja wakati Rais Trump akiendelea kutokuungwa mkono kwa sera zake, ambapo fainali za mwaka huu zikiahuhudia baadhi ya wachezaji, viongozi na mashabiki wakizuiwa kuingia Marekani.

Related articles

Recent articles