23.6 C
New York

Wakala afunguka Salah kutimkia Uturuki

Published:

MERSEYSIDE, Uingereza

WAKALA wa Mohamed Salah, Ramy Abbas Issa, ameibuka na kukanusha taarifa zinazodai kuwa mshambuliaji huyo amekubali kujiunga na Besiktas ya Ligi Kuu nchini Uturuki.

Abbas Issa amesema si kweli na mpaka sasa hakuna mwafaka waliofikia juu ya klabu atakayocheza Salah msimu ujao.

Kupitia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X, wakala huyo ameongeza: “Binafsi sijui Salah atacheza wapi msimu ujao. Siyo kawaida yetu kuzungumza na klabu ambayo Salah haitaki.”

Salah aliondoka Liverpool mwishoni mwa msimu uliopita (2025-2026) na hivi karibuni alikuwa na kikosi cha timu yake ya taifa ya Misri katika fainali za Kombe la Dunia.

Kama itakumbukwa, Mafarao hao ambao wanaongoza kwa kutwaa taji la AFCON, waliishia hatua ya mtoano baada ya kufungwa mabao 3-2 na Argentina ya Lionel Messi.

Related articles

Recent articles