22.7 C
New York

Kris Jenner atangaza kifo cha ‘bi mkubwa’ wake

Published:

LOS ANGELES, Marekani

MAMA mzazi wa mrembo anayetokea familia ya Kardashian, Kris Jenner, Mary Jo, amefariki akiwa na umri wa miaka 91.

Kris (70), ndiye aliyetangaza kifo cha ‘bi mkubwa’ wake huyo akisema: “Leo tumemuaga mama yetu kipenzi MJ …”

Mary Jo amekuwa na umaarufu mkubwa nchini Marekani kwa kuonekana mara kwa mara kwenye kipindi cha televisheni cha ‘Keeping Up With The Kardashians’.

Mbali na Kris, pia mama huyo ana mtoto aitwaye Karen Houghton, ambaye hata hivyo alifariki Machi, 2024, akiwa na umri wa miaka 65.

Amefariki na kuacha wajukuu sita; Kourtney (47), Kim (45), Khloe (42), Rob Kardashian (39), Kendall (30), na Kylie Jenner (28).

Related articles

Recent articles